SUMU YA PENZI SEHEMU YA SABINI NA SITA (76)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Basi ili kufanya mpango usishtukiwe Yule daktari akamlaza baba pale hospitali na kumuandikia dozi za uongo ili kuonekana kama kweli alikuwa amewekewa sumu. Mimi peke yangu ndiyo nilikuwa najua nilichokifanya, tukarudi nyumbani na Mage na mwanangu.
Tulipofika tu, nilimkuta mume wangu amekaa kwenye kochi akionekana na mawazo mno, aliponiona tu naingia alikuja na kunikumbatia, mtoto wa kiume akiangusha chozi bila aibu.
Akambeba mwanaye kwa mapenzi makubwa na kunichukua tukaenda kukaa pale nje kwenye ule uwanja wetu, akaanza kuniomba msamaha kwa yote yaliyotokea lakini alionekana muoga mno hata kukaa dakika chache tu za ziada nchini. Alitaka tuondoke.
Ikabidi nimuelezee kisa kizima kilichotokea pale airport nikamdanganya kuwa Hadija alikuwa amebeba madawa ya kulevya, sikumtajia kabisa kama mimi ndiye niliyemuwekea.Akashangaa na kumshukuru Mungu kwa yote yaliyotokea.
Basi kukamilisha furaha yake nikamuelezea pia kuhusu ishu ya baba ilivyotokea, akastaajabu mno lakini hata huko sikumtajia kama mimi ndiyo nilichonga na Daktari kuwa afanye manuva kuhusu baba aliwekewa sumu na Fatuma.
“Nisamehe sana mke wangu..nitalipia kila ulichokifanya kwa ajili yangu..nakupenda sana.” alisema kwa sauti na kunikumbatia kwa nguvu, nilihisi alikuwa akilipia kwa muda wote aliokuwa mbali na mimi.


UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA


ITAENDELEA JUMAPILI.
Post a Comment
Powered by Blogger.