SUMU YA PENZI SEHEMU YA SABINI NA SABA (77)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


“We Mary vipi?” alinishtua dada Mage nikazinduka kutoka kwenye mawazo yangu.
“Sikia Mage haina haja ya wewe kuniviziavizia ovyo kama unavyofanya, italeta picha mbaya. Cha msingi nitakuwa nakufundisha mambo kadhaa ninayoyajua,” nilimwambia Mage nikashangaa kumuona mwenzangu akiripuka kwa furaha sana kama vile nimemtangazia dili la mabilioni ya fedha.
“Tunaanza lini? niambie nipo tayari hata sasa hivi..” alisema Mage akionekana yupo haihai.
“sikia Mage, wewe mwenyewe unajua masahibu yaliyotukuta hivi karibuni lakini ngoja nina kidaftari nimeandika vitu vyote nilivyofundishwa zamani.” “Ulifundishwa? Wapi tena huko mwalimu wako alikuwa nani?”
“ooh ni stori ndefu lakini mwalimu wangu mkubwa alikuwa ni huyuhuyu mume wangu..” “Ha! Kwani mlikutanakutana vipi?” aliuliza kwa shauku Mage ikabidi nimhadithie mkanda mzima, wale waliosoma hadithi ya Mr X part One wataelewa hapa.
Basi akazidi kujaa hamu basi nikaingia chumbani na kuchukua kile kidaftari changu nilichokuwa nikiandikiaga mafunzo yote ya darasani kipindi kile na kumkabidhi nikamwambia akisome na kufanya kwa vitendo kila kitu.
Huwezi amini hiyo ndiyo ilikuwa kama tiketi kwa dada kuondoka jikoni na kwenda kukisoma kile kijidaftari. Nilijuta maana kazi zote siku hiyo zilinidondokea mimi . 


UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA

ITAENDELEA JUMATATU.
Post a Comment
Powered by Blogger.