SUMU YA PENZI SEHEMU YA SABINI NA NNE (74)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


“Ha! Mama hii aliandika lini? Kwani ni baba huyu au?” niliuliza kwa mshangao.
“ndiyo ni mwandiko wa baba yako, nahisi aliandika juzi alipokuja baada ya kumuita kwenye mshumaa na kumwaga chumvi nje!” alisema mama kwa woga.
“Mh jamani mimi mbona sielewi?” aliuliza dada.
“yaani hapa kama ni juzi basi inaonekana alipoingia ndani akili yake ilirudi, halafu wakati mvua inaanza kunyesha na kuyeyusha chumvi kule nje ndiyo akaanza kupagawa na kuandika huu ujumbe,” nilisema huku nguvu ya hoja yangu ikiwa wazi kabisa kwenye maandishi ya baba. “Jamani kama kweli baba ndiyo kaandika huu ujumbe juzi basi ndiyo hatuna kitu tena, maana Fatuma atakuwa ndiyo ameandikwa kwenye mirathi,” alisema Mage.
“hapana lazima tupiganie tumpate baba kwanza, mirathi itaandikwa tu upya.” Nilisema.
“Na ndiyo tukimpata akiwa hai, we unafikiri kama kashaandika mirathi, Fatuma atamuacha baba hai?” alisema Mage nikamuangalia mama akipiga magoti na kusali, nikaangalia tena ule ujumbe na kugundua kuwa baba ameandika namba ya mwanasheria wake.
“Mama, mwanasheria wa baba unamjua?” nilimuuliza mama aliyeonekana amechanganyikiwa mno.

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA

ITAENDELEA IJUMAA
Post a Comment
Powered by Blogger.