Ratiba ya robo fainali ya kombe la FA imetoka, Mourinho uso kwa uso na Conte

Ratiba ya kombe la FA katika hatua ya robo fainali imetoka baada ya kufanikiwa kuvuka katika hatua ya raundi ya tano. Sasa kombe hilo limeanza kuwa na mvuto baada ya timu ya Manchester United inayoongozwa na Jose Mourinho ikipangiwa kukutana na Chelsea ya Antonio Conte katika hatua hiyo.

Man United imefanikiwa kuingia katika hatua hiyo baada ya kuifunga Blackburn Rovers 2-1 Jumapili hii huku Chelsea wakiibuka kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wolves Hampton. Hii ni ratiba ya mechi za robo fainali ya kombe hilo ambapo zinatarajiwa kuchezwa kati ya Machi 11 na 12 ya mwaka huu.


Chelsea vs Manchester united
Middlesbrough vs Huddersfield & Man City
Tottenham Hospurs vs Millwall
Lincoln City vs Arsenal & Sutton Uni
Post a Comment
Powered by Blogger.