PICHA: TID, RECHO NA WENGINE WATUA MAHAKAMA YA KISUTU

Wasanii hao wakiwa mahakamani. 

Wasanii akiwemo TID, Recho,  Tunda na baadhi ya watu wanaoshikiliwa na kituo cha polisi kati kwa tuhuma ya dawa za kulevya wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Watuhumiwa hao wameshushwa nyuma ya majengo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku baadhi ya wakijifunika nyuso zao kukwepa camera za mapaparazi.
Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi iliyotolewa Jumatatu hii ilidai watuhumiwa 12 watasomewa kiapo cha kutorudia Matumizi ya Madawa ya kulevya na kuwa katika uangalizi wa mahakama na jeshi la polisi kwa miaka 2.
Aidha jeshi hilo lilidai baada ya kiapo hicho watuhumiwa wawili kati ya hao watarudishwa polisi aliwemo Wema Sepetu kujibu tuhuma za kukutwa na msokoto wa bangi.
Post a Comment
Powered by Blogger.