Mvua yasababisha mawasiliano kukatika wilayani Monduli

Mvua zilizoanza kunyesha wilayani Monduli mkoani Arusha zimesababisha  mawasiliano ya  barabara   katika  baadhi ya maeneo ya  wilaya  hiyo  kukatika, baadhi ya wananchi kukosa huduma na pia wanafunzi kushindwa kwenda shule  kutokana  na   baadhi  ya mito  kufurika.
Wananchi na viongozi wa maeneo yaliyoathiriwa  na hali hiyo wamesema   tatizo  hilo  ni   la  muda  mrefu   na  ni  jambo  la  kawaida  wakati  wa  msimu  wa  mvua  unapoanza na  ni kubwa  zaidi  katika  tarafa ya  Makuyuni.

Hali  hiyo  pia  imeshudiwa  na  viongozi  watendaji   na  wataalam   wa  wilaya  na  mkoa   ambao  walilazimika  kukatisha  safari  ya kwenda  kusikiliza  kero  za   wananchi  wa  kijiji  cha Oltukai   wanaokabiliwa  na  matatizo  mbali  mbali  likiwemo  tatizo  la  maji.

Wakizungumzia  hali  hiyo  viongozi  hao   akiwemo  mkurugenzi  mtendaji  wa  halmashauri  ya  Monduli  Bw.  Steven  Ulaya  na  mwenyekiti  wake  Bw.  Issack Joseph  wamesema   tatizo  hilo  ni  kubwa  katika  wilaya hiyo   na kwamba  wanafunzi  wote  wanalazimika  kulala  shuleni.

Baada  ya  msafara  wake  kukwamishwa  na  mafuriko hayo  mkuu  wa  mkoa  wa  Arusha Mrisho  Gambo   amewataka  watendaji   wa  halmashauri  hiyo  wakiwemo   watalaam   kuanda  mpango wa  muda  mrefu   wa  kukabiliana  na  hali  hiyo  ili kuepuka  madhara  yasiyo  ya lazima.
Post a Comment
Powered by Blogger.