MTOTO WA DARASA LA NNE AFANYIWA UKATILI KWA KUCHOMWA MOTO MIKONO JIJINI DAR ES SALAAM

Bi.Tatu Rashid mkazi wa Kivule jijini Dar es Salaam amemfanyia ukatili mtoto wake wa kumzaa kwa kumfunga mikono yake miwili,kisha kumuwekea mifuko ya plastiki na kumchoma moto baada ya mtoto huyo kudaiwa kuchukua shilingi 1000.
Tukio hilo la kikatili alilofanyiwa mwanafunzi wa darasa la nne jina linahifadhiwa, limetokea jana eneo la Kivule jijini Dar es Salaam,ambapo ITV baada ya kubaini ukatili huo ilifuatilia sakata hilo na kukuta suala hilo likiwa limefikishwa katika ofisi ya serikali ya mtaa wa huo, ambapo mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne ameeleza kwamba licha ya licha kumuomba msamaha mama yake mzazi kwa kuchukua shilingi 600 bila kumuomba lakini mama yake hakumuhurumia na badala yake alilazimisha kuwa kachukua shilingi 1000 jambo ambalo limemuhuzunisha baba mzazi wa mtoto ambaye hakuwepo nyumbani wakati wa tukio.

Majirani wa familia hiyo wamesema mama huyo baada ya kuona mtoto wake atagundulika kachomwa moto alijaribu kumfungia ndani tangu jana lakini walishirikiana na kutoa taarifa baada ya kuhuzunishwa na tukio hilo.

Mama wa mtoto huyo Bi. Tatu Rashid amekiri kumfanyia mtoto huyo ukatili huo baada ya mtoto kuiba shilingi 1000 lakini akadai eti hakukusudia huku uongozi wa mtaa huo ukidai wanampeleka mama huyo kituo cha polisi huku mtoto huyo anapelekwa hospitali.

CHANZO: ITV TANZANIA
Post a Comment
Powered by Blogger.