Mbwana Samatta aumia Genk ikipoteza mbele ya KV Oostende

Samatta akitoka nje baada ya kuumia

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta wa klabu ya KRC Genk amejikuta katika wakati mgumu usiku wa Jumanne hii wakati timu yake ya KRC Genk ilipokuwa ikicheza na KV Oostende katika mchezo wa kombe la Ubelgiji.
Samatta aliumia katika daika ya 23 na kulazimika kutolewa nje ya uwanja na kumpisha Jose Naranjo ambaye alikosa p3enati katika mchezo huo.
Katika mchezo huu ambao Genk walikuwa katika uwanja wao wa nyumbani Luminus Arena walijikuta wakipoteza mchezo huo kwa kufungwa goli 1-0 dhidi ya KV Oostende na kutolewa katika kombe hilo huku goli hilo likifungwa dakika ya nane na Knowledge Musona ambaye ni raia wa nchini Zimbabwe.
Post a Comment
Powered by Blogger.