MAMA WEMA AZIDIWA BAADA YA KUMWONA MWANAE SENTRO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mama Mzazi wa Wema Sepetu akitoka katika kituo cha kati jijini Dar es Salaam alipokuwa ameenda kumuona mwanaye..

MAMA mzazi wa Wema Sepetu, Mariam Sepetu amezidiwa baada ya kupandwa na presha wakati alipokwenda katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar (Sentro) kwa ajili ya kumuona mwanaye ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi pamoja na wasanii wenzake kwa tuhuma za kuhusika na mtandao wa matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya.
Katika hali hiyo, mama Wema aliishiwa nguvu na kusaidiwa na ndugu wawili waliokuwa wameambatana naye kituoni hapo na kutolewa nje ya lango kuu la kituo hicho kisha muda mfupi baadaye akaonekana akiondoka eneo hilo
Post a Comment
Powered by Blogger.