MAHAKAMA YATUPA RUFAA YA KUPINGA KESI YA UCHAGUZI JIMBO LA LONGIDO

Mahakama ya Rufaa nchini imetupilia mbali rufaa ya kupinga hukumu ya kesi ya uchaguzi katika jimbo la Longido mkoani Arusha.
Uamuzi huo umesomwa leo (Alhamisi) na msajili wa Mahakama ya Rufaa nchini, Amir Msumi na kusema kwamba wakata rufaa waliwasilisha rufaa mpya badala ya kurekebisha baadhi ya vipengele kama walivyoagizwa na mahakama.
Msumi amesema badala ya kuwajumuisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali na msimamizi wa uchaguzi kwenye rufaa hiyo, wakata rufaa walifanya kitu ambacho hawakuruhusiwa kukifanya na mahakama na hivyo rufaa hiyo imetupwa na wanapaswa kulipa gharama za uendeshaji wa kesi hiyo.
Post a Comment
Powered by Blogger.