Luteni Jenerali Herbert ateuliwa kuwa mshauri mpya wa usalama Marekani

 Rais wa nchi ya Marekani, Donald Trump amemteua Luteni Jenerali Herbert Raymond McMaster kuwa mshauri mkuu wa ikulu kuhusu masuala ya usalama wa taifa.

Luteni Jenerali Herbert anachukuwa nafasi hiyo ambayo hapo awali ilikuwa ikishikiliwa na Michael Flynn ambayue alijiuzulu wiki iliyopita baada ya kufanya kazi hiyo kwa wiki tatu tangu alipoteuliwa na Trump.
Flynn alijiuzulu February 13 huku tatizo kubwa likiwa ni kutoa taarifa zisizokuwa na ukweli juu ya mkutano wake na balozi wa Urusi.
Aidha Herbert amewahi kufanya kazi katika jeshi la Marekani nchini Iraq na Afghanistan kalini pia ni msomi wa masuala ya historia kutoka chuo kikuu cha North Carolina.
Post a Comment
Powered by Blogger.