JAJI FATUMA HAMISI MASENGI AAGWA RASMI MAHAKAMA KUU KANDA YA ARUSHA LEO

Na.Vero Ignatus.
Sherehe za kumuaga aliyekuwa Jaji mfawidhi wa mahakam kuu kanda ya Arusha Mhe,Fatuma Hamis Masengi ,zimefanyika leo katika mahakama kuu ya ndanda hiyo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo majaji,mahakimu,mawakili wasajili wa mahama watendaji pamoja na wageni waalikwa.

Sherehe  hizo zimeanza majira ya saa asubuhi katika mahakama ya wazi ambapo Jaji Fatuma alianza kufanya kazi mnamo mwaka 1974 katika mahakama ya mwanzo na kuendelea kuitumikia mahakama hadi alipoteuliwa kuwa jaji mfawidhi mahakama kuu.

Amewataka majaji na mahakimu pamoja na wale wote wanaofanya kazi za kimahakama wafanye kazi kwa kumtegemea Mungu huku wakijua kazi yeyote ina changamoto zake hivyo ni vyema kufanya kazi kwa weledi zaidi na kwa kuzingatia sheria inavyosema,wakimtendea haki kila mtu kwa stahiki.

Amewataka wanawake kutokukata tamaa huku akisema kuwa wanawake wanaweza kuliko wanaume japo kuwa wakati mwingine wanaume wanaona kama vile wanawake ni wanyonge lakini mwanamke anaweza pale ambapo anasimama kwa nafasi yake na kulitumikia kusudi kwa wakati na weledi.

"Wanawake  wenzangu msikate tamaa na kujiona wewe ni dhaifu ,tunaweza msibweteke unapopata nafasi itumie vizuri bila kuaharibu taratibu zilizowekwa ,fanya kazi kwa bidii na jamii itaona juhudi zako ,wanawake tunaweza "alisema masengi.
Aidha Jaji  Fatuma amesema kuwa anamshukuru sana Mungu kwa kumuwezesha kwa wakati wote ambapo amekuwa akifanya kazi yenye majukumu  mazito, amezishukuru Asasi za kiserikali na zile zisizo za kiserikali,amewashukuru wale wote walioshirikiana nae katika kipindi chote alichokuwa akitimiza majukumu yake ya kikazi.
Waheshimiwa majaji kanda ya Arusha na Kilimanjaro wakiwa kwenye picha ya pamoja,Wakwanza kulia ni Mh Jaji Dkt.Modesta Opiyo,Wakwanza kushosto ni Mhe. Jaji Salma Maghimbi. Picha na Vero Ignatus Blog.
Mhe. Jaji Mstaafu wa mahakama kuu kanda ya Arusha Fatuma Hamis Masengi akiwa kwenye picha ya pamoja na waheshimiwa mahakimu wa mahakama ya mwanzo mahakimu hao wamelelewa na Mhe Fatuma Masengi.

Post a Comment
Powered by Blogger.