ZAIDI YA WATU LAKI TISA WASAINI KUPINGA ZIARA YA TRUMP UINGEREZA

 Zaidi ya watu 900,000 wamesaini petition ya kutaka kusitishwa kwa ziara ya Donald Trump nchini Uingereza kufuatia uamuzi wake wa kupiga marufuku waislamu kuingia Marekani.

Na sasa wabunge wa House of Commons watalazimika kujadili ziara hiyo.

Mipango ya Trump kuzulu nchini Uingereza, ilitangazwa saa 48 zilizopita baada ya waziri mkuu, Theresa May kueleza kuwa Rais huyo ameukubali mwaliko toka kwa malkia.

Petition hiyo inadai kuwa Trump hapaswi kualikwa nchini humo kuepuka kumdhalilisha malkia. Uamuzi wa Trump kuzuia raia wa nchi 7 za Kiislamu kuingia nchini Marekani umepingwa vikali.
Post a Comment
Powered by Blogger.