WATU 39 WAUAWA SIKU YA MWAKA MPYA KWENYE KLABU YA USIKU INSTABUL

Ndugu wakiwa kwenye mazishi ya Ayhan Arik, mhanga wa tukio la mauaji kwenye klabu ya usiku ya Reina, Istanbul, Ururuki, January 1, 2017. REUTERS/Osman Orsal
Mtu aliyekuwa na bunduki aliwafyatulia risasi watu waliokuwa wakisherehekea mwaka mpya kwenye klabu ya usiku mjini Istanbul, Uturuki na kuua 39, Jumapili. Miongoni mwa waliopoteza maisha wamo raia wengi wa kigeni.

Baadhi ya watu wamejeruhiwa baada ya kuruka ili kujiokoa kufuatia mtu huyo kuanza kumwaga risasi hovyo kwenye klabu ya Reina, saa chache tu baada ya mwaka mpa kuingia.
Kusudi la shambulio hilo bado halijabainika lakini kuna uwezekano likawa limefanywa na kundi la Islamic State ambalo limehusishwa na matukio mengi ya kigaidi nchini humo mwaka jana.
Post a Comment
Powered by Blogger.