WACHIMBAJI WALIOFUKIWA NA KIFUSI WASEMA WAKO HAI

Wakati  imeelezwa kuwa waokoaji katika mgodi wa dhahabu wa RZ Union ulioko Geita , wamebakiza mita tatu kuwafikia waliofukiwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Medard Kalemani akizungumza na ndugu wa watu waliofukiwa amesema kwamba wanafanya mpango wa kuwapelekea chakula wachimbaji hao.
Amesema kwamba jana wamefanikiwa kufanya mawasiliano na wachimbaji hao na kwamba wapo kumi na watano na kuwa wanachohitaji kwa sasa ni chakula.

Alisema waokoaji walifanikiwa kuwafikishia kamba na kalamu watu hao ambao waliandika majina  na  mahitaji yao na kusema kwamba wote wapo salama.

Watu hao akiwemo raia wa China mmoja walifukiwa na kifusi juzi usiku baada ya udongo kukatika na kuziba mlango waliokuwa wakitumia kuingia na kutoka na uokoaji unaendelea kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya uokoaji.

Watu wengi wapo katika eneo hilo wakiwemo ndugu wa waliofukiwa lakini kwa juhudi wanazoziona za uokoaji wametulia na kufuata maelekezo wanayopewa ikiwemo kukaa mita 500 toka eneo la tukio.

Post a Comment
Powered by Blogger.