VIDEO: TUNDU LISU AFUNGUKA BAADA YA MBUNGE WA CHADEMA KUFUNGWA MIEZI SITA

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amesema kuwa chama hicho kinafanya juhudi za kukata rufaa katika kesi ya Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali aliyefungwa jela miezi sita.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za chama hicho, Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki alisema Lijualikali ameanza kupigwa vita na serikali mara tu baada ya kuwa diwani wa kata ya Ifakara, mwaka 2012.
Alisema Chadema kitafanya juhudi za kukata rufaa na kumtafutia dhamana Lijualikali baada ya jana kuhukumiwa kifungo hicho

CHANZO: MWANANCHI
Post a Comment
Powered by Blogger.