UPDATES: WACHIMBAJI 14 WAFUKIWA NA KIFUSI NYARUGUSU

Wachimbaji wadogo 14 kutoka mgodi wa dhahabu wa RZ uliopo Kata ya Nyarugusu mkoani Geita wamefukiwa na kifusi cha udongo baada ya kutokea maporomoko kwenye moja ya shimo walilokuwa wanachimba.
Watu hao ni raia 13 Watanzania na raia mmoja wa China. Tukio hilo limetokea saa 9 usiku leo wakati wachimbaji hao wakiendelea na shughuli ya uchimbaji katika mgodi wa RZ unaomilikiwa na wachina.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga ametembelea eneo la tukio na kuona shughuli za uokozi zikiendelea na kuagiza nguvu ziongezwe
Post a Comment
Powered by Blogger.