MATANGAZO....
pamoja blogBABA

HABARI

MATUKIO

Michezo imedhaminiwa na

MICHEZO

Simulizi zimedhaminiwa na

SIMULIZI

JAMII

BURUDANI

UCHUMI

MAGAZETI

VIDEO ZETU

» » » » » UPDATES: MOTO WATEKETEZA JENGO LA MAKAZI YA ASKARI POLISI MJINI MOSHI


Pamoja Blog 1/26/2017 04:00:00 AM 0

Moto mkubwa ambao chanzo chake bado hakijafahamika, umeteketeza jengo la ghorofa mbili la makazi ya Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) la mjini Moshi usiku huu.
Vikosi vya zimamoto na uokoaji kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Moshi na Kiwanda cha Sukari cha TPC vilikuwa vikiendelea na jitihada za kuuzima moto huo.
Mashuhuda wameliambia gazeti hili kuwa moto huo umeanza saa 2: na hadi kufikia saa 4:00 ulikuwa umeteketeza ghorofa ya pili unakosadikiwa kuanzia.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa familia zote za askari wa kikosi hicho cha FFU wanaoishi katika nyumba hiyo wamefanikiwa kutoka salama isipokuwa baadhi ya mali zimeteketea.
Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia jitihada kubwa zikifanyika za kuuzima moto huo lakini unaonekana kuzidi kushika kasi baada ya gari la Halmashauri kuishiwa maji.
Hii ni mara ya pili kwa jengo hilo kuungua moto, miaka ya hivi karibuni lililipuka moto na vikosi vya zimamoto vilifanikiwa kuudhibiti.
Sehemu ya Familia za Askari waliokuwa wakikaa katika Jengo hilo pamoja na mashuhuda wakiangalia tukio hilo wakati vikosi vya Zimamoto na Uokoaji vikiendelea na jitihada za kuudhibiti moto huo.
Sehemu ya mali zilizoteketea kwa moto huo.
Jitihada za kuuzima moto huo kwa baadhi ya maeneo ndani ya jengi hilo zikiendelea.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments