UPDATES: DK. ANNA CLAUDIA SENKORO AFARIKI DUNIA

Dk Senkoro ambaye ni mwanamke wa kwanza katika historia ya nchi kugombea Urais kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2005 kupitia Chama cha TPP – Maendeleo, alifariki dunia ghafla leo (Jumatano) asubuhi wakati akipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu.
Msemaji wa Taasisi ya hiyo iliyopo Muhimbili, Maulid Kikondo amesema Dk Senkoro alifika hospitalini hapo jana saa 10.0 jioni kwa ajili ya matibabu na kufanyiwa vipimo kadhaa ambavyo madaktari waligundua tatizo lililokuwa likimsumbua.
Kikondo amesema baada ya vipimo alishauriwa kulazwa kutokana na hali yake, lakini Dk Senkoro alikataa na kutaka kurudi nyumbani.
Post a Comment
Powered by Blogger.