TANESCO: MABADILIKO YANAYOFANYIKA HAYANA MWISHO

Kaimu Mkurugenzi wa shirika la umeme Tanzania (Tanesco) amesema mabadiliko yanayoendelea yakilenga kuimarisha uongozi na kuimarisha ufanisi wake hayana kikomo.

Mkurugenzi huyo ameyasema hayo Jumapili hii kwa njia ya simu na mwandishi wa Mwananchi kwamba kazi hiyo itazidi kuendelea kwa muda usiojulikana na kusema kuwa shirika haitabakiza mtu yoyote asiye na sifa.
“Mabadiliko haya, kama ambavyo mmeona tulivyoanza huko nyuma, hayana mwisho. Tunapitia maeneo yote ndani ya shirika na hatutaacha sehemu yeyote, mahali popote tukiona kuna haja ya kufanya mabadiliko,” alisema Mwinuka.
Mkurugenzi huyo alipoulizwa kuhusu eneo la dharura linalolalamikiwa na zaidi na wateja alisema kuwa hilo ni sehemu ya maeneo ambayo yanashughulikiwa na kuongeza kwa kusema kuwa si kazi ya siku moja
Hivi karibuni Rais Dkt John Magufuli alitengua uteuzi wa Mhandisi Felchesmi Mramba aliyekuwa Mkurugenzi wa shirika hilo.

Post a Comment
Powered by Blogger.