SUMU YA PENZI SEHEMU YA SITINI NA TATU (63)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


“Haya njoo basi nje tuongee,” nilisema nikijiandaa kumuita Hadija nje, lakini mume wangu akainuka yeye kabla na kusema tuendelee na maongezi wakati yeye akienda nje.
“haya niambie vipi bibi wewe kimguu chako hadi kwetu! nimesikia mambo yako naona unanitafuta kwa nguvu sana,” nilianza kumpa vipande vyake.
“ha! Jamani Mary mimi nakutafuta kwanini?” alijifanya kushangaa eti.
“wewe siyo wa kumtongoza mume wangu, halafu nakushangaa unaniibia hadi chupi zangu kisa na mkasa ni nini? kwa taarifa yako haunipati mimi wala mume wangu,” nilimkoromea, kwa maneno hayo nikitarajia asirudi tena nyumbani kwetu.
“shoga utakuwa umechanganya mambo, tafadhali nisikilize basi na mimi, kiukweli chupi yako niliipenda nikaona niichukue baadaye nikwambie, mwenzako siku ile yangu niliichafua halafu nilikuwa naenda kukutana na shemeji yako, si unajua tena sisi wanawake.” Alisema bila haya Hadija.
“Ha! ndiyo univalie chupi yangu, kweli hiyo ndiyo nasikia leo. kwa hiyo nguo za watu za ndani nazo mnavaliana?” niliuliza kwa mshangao.
“siyo hivyo, lakini nisamehe tu Mary nimekuwa siyo mstaarabu, halafu mumeo mwenyewe mbona ndiyo ananiitaga nije!”
“weee ishia hapohapo kenge wee! Najua kila kitu, kwa taarifa yako ananieleza uchafu wako wote, siyo mwanaume wa kibongo yule eti awe mwongomwongo, nimemtuliza na yeye ametulia. Sasa kuanzia leo sitaki kukuona karibu yangu sitaki urafiki na wewe na unikome umesikia! Bitch jus get out!” nilifoka kwa hasira kweli.


UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA

ITAENDELEA JUMATATU
Post a Comment
Powered by Blogger.