SUMU YA PENZI SEHEMU YA SITINI NA SITA (66)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Basi huwezi amini nilikaa lumande katika kile kituo kidogo cha polisi nikiwa na mawazo, hofu, hasira na majuto vyote kwa pamoja; ombea isikukute hali hiyo.
Ilipofika kesho yake asubuhi nikachukuliwa na karandinga la polisi hadi mahakama ya mwanzo ya Sinza ili kusomewa kwa mara ya kwanza mashtaka yangu.
Nikasomewa mashtaka mbele ya hakimu mama mtu mzima kidogo, kuwa tarehe deshideshi nilienda kwa mshtaki, Hadija Stambuli na kumshambulia mwili na kumjeruhi. Nikapangiwa tarehe ya kusikiliza utetezi wangu kuwa ni wiki ijayo.
Basi nikapandishwa mabasi ya wafungwa na pingu zangu hadi gereza la Keko. Ni kumbukumbu mbaya ambazo sitawahi kuzisahau maishani mwangu. Kisa cha hayo yote eti ni mapenzi.
Nikiwa jela mara kadhaa mama na dada walikuwa wakija kunitembelea, lakini si baba wala mume wangu aliyekuja, kila siku mama alionekana kuwa na huzuni mno kuzidi hata mimi niliyekumbwa na majanga. Moja kwa moja nikajua kuwa lazima kuna kitu kinaendelea na hataki kuniambia. Ikabidi nimuombe dada anielezee kitu gani kinamtatiza mama.
Akaniambia bila kificho kuwa tangu niwekwe korokoroni, mume wangu hajakanyaga nyumbani na ameondoka na mtoto wangu ndiyo maana mama yupo vile. Mungu wangu! Hadija alivyo mchawi si atanigeuzia mwanangu ndondocha!
Akili ziliniruka mno, nikawa namlaumu Mr X kwa nini ananisaliti, nikasahau kabisa kuwa ni limbwata.

\UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA


ITAENDELEA ALHAMISI
Post a Comment
Powered by Blogger.