SUMU YA PENZI SEHEMU YA SITINI NA TANO (65)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Nililala usiku mzima nikiwa na hofu asubuhi mapema niliamua kwenda kwa Bi. Gululi lengo langu nimuelezee yaliyonikuta kwa mume wangu kama alikuwa na maelezo yoyote ambayo yangeweza kunituliza.
Baada ya kufika nikamkuta Bi Gululi akiwa na Gululi, nikawapa mkanda mzima. Gululi akawa anasikitika tu.
“Mwanangu, kwanza kuzaliwa, pili ni mapenzi tatu ni kifo. Kwa umri wangu huu japo sijakula chumvi za kutosha, nimeona mengi mno, nimeshuhudia maajabu kwenye mapenzi; mengine yanaelezeka, lakini kuna yale yasiyoelezeka ambayo naamini kabisa kuwa uchawi unahusika,” alisema Bi Gululi.
“uchawi? Una maanisha Hadija kanirogea mume wangu!” nilisema kwa wasiwasi.
“mwanangu, kwa niliyoyasikia ya kuanza kuibiana chupi, na kuja nyumbani kwako kumpikia mumeo, hapo kuna tatizo ni limbwata tu hakuna kitu kingine,” alisema Bi Gululi nikazidi kuogopa kwasababu hakuwahi kuamini uchawi kirahisirahisi.
“Kwa hiyo bibi nafanyaje sasa,” nilimuuliza Bi Gululi nikitarajia msaada wowote.
“Gululi, hebu msaidie mwenzako wewe ndiyo unajua hayo mambo yenu,” alisema Bi Gululi nikashangaa kwanini alimpa mwanaye ndiyo anijibu cha kufanya.
Basi na yeye kabla hajasema chochote, akaanza kunilaumu kuwa alishanionya lakini sikusikia. Nilikaa kimya tu.


UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA

ITAENDELEA JUMATANO
Post a Comment
Powered by Blogger.