SUMU YA PENZI SEHEMU YA SITINI (60)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


“Hallow Mr Jermaine. Me is seeing you there. Is the morning great! Is’nt it” aliongea kwa kuungaunga, basi mimi kuona tu sura yake alikuwa ameshanitumbukia nyongo, nikaamua kuingia zangu ndani na mwanangu.
Kichwani nikiwaza nitamkomoaje baba, na huyo Fatuma wake ili waachane? Sikupata jibu.
Ilipofika mchana hivi wakati tunaandaa chakula, mimi nikatoa wazo kwa wenzangu kuwa tungeenda familia nzima ufukweni kubarizi, na hasa kumtembeza mama ambaye alizoea tu kukaa nyumbani.
Wazo hilo likaonekana kufurahiwa mno hasa na dada yangu Mage, basi mida ya saa tisa tu, tulikodi taksi na kuondoka zetu tukielekea Kawe, tukiitafuta bichi ya Piccolo Hoteli.
Tulitulia hapo huku kila mtu akivinjari kwa mtindo wake, mimi vile ninavyoyapenda maji, nilirukia kwenye swimming pool na nguo zangu za kuongelea nikawa nashindana na dada nani atamshinda mwenzake kufika kulee na kurudi huku mwanzo.
Tukawa tunaenda mwanzo hadi mwisho, lakini kote huko mimi nikiibuka kidedea. Mchezo mzima ukawa unaboa maana kila saa nilishinda mimi tu. Basi tukapiga mapicha ya kutosha, nyingine nikaomba dada Mage anipige nikiwa nimebebwa na mume wangu na mapozi kibao ya aina hiyo.

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA

ITAENDELEA IJUMAA
Post a Comment
Powered by Blogger.