SUMU YA PENZI SEHEMU YA SABINI NA MOJA (71)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.“fungua hapo chini ya ua,” aliposema hivyo nikainua lile ua lililopandwa ndani ya ndoo na kuchukua ule ufunguo. Nikafungua  na kuingia ndani kweli nikakuta kuna nguo mpya nzuri Hadija amenunuliwa, kweli safari ilikuwa imeiva. Nikaona mabegi nikatoa nguo zangu za ndani lakini nikapata wazo, nikaona ngoja niziache. 
Nikaanza kutafuta hilo limbwata linapowekwaga, nikafungua chini ya mto, sikuona kitu, nikafungua chini ya godoro, sikuona kitu, nilipoangalia chini ya kitanda nikaona kuna chetezo nikakivuta na kuona ndani yake kuna makaa na jivu, lakini cha ajabu chetezo kilikuwa hakinukii udi. Nikaangalia vizuri tena chini ya kitanda nikaona kuna vifundo vya mifuko ya nailoni, nikavichukua na kuvifungua ndani , nikashangaa kuona kuna kifuko kimoja kina ile chupi yangu  nyekundu ikiwa imecharangwacharangwa vipande vingi.  halafu kile kingine kilikuwa na mavumbivumbi nisiyoyafahamu.
Hapo nikajua kuwa Hadija huwa anachukua kipande kimojakimoja nakuchanganya na hayo mavumbi mengine na kujifukiza ili mradi atembelee nyota yangu. kwa nilichokiona nikakubali kuwa kwa uchawi simuwezi lakini siyo kwa akili. Nikapanga mpango.
Nikatoka nje, kwanza maana yule mama alikuwa akinisubiria mlangoni.
“vipi tayari!” aliniuliza akionekana ana haraka mno ya kunitaka nifunge mlango na kuondoka.

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA

ITAENDELEA JUMANNE
Post a Comment
Powered by Blogger.