MATANGAZO....
pamoja blogBABA

HABARI

MATUKIO

Michezo imedhaminiwa na

MICHEZO

Simulizi zimedhaminiwa na

SIMULIZI

JAMII

BURUDANI

UCHUMI

MAGAZETI

VIDEO ZETU

» » » SUMU YA PENZI SEHEMU YA SABINI (70)


Pamoja Blog 1/29/2017 11:00:00 AM 0

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Usiku ulipoingia nikaanza kuhesabu maumivu, nikalala nikiwaza nifanye nini, nikatamani kumpigia simu Hadija nimuombe radhi, nikatamani kwenda kwa yule mganga aliyenipeleka Gululi nikaombe anisaidie na hata kama atataka nimpe penzi nifanye hivyo. Nikawaza kwenda kwa mchungaji, mawazo yote hayo yalinijaa tele.
Nikaona jambo la kwanza kufanya ni kumpigia simu kwanza Hadija hata kumpigia magoti nifanye tu, maana kanigusa kunako, hata kama atataka hela yoyote mimi nitampa ili mradi tu anipe mume wangu.
Wakati nawaza hayo kuna kitu kikaniambia niangalie kwanza  whatsapp namba ya Hadija, nikaona kuna picha moja ameipiga ndani ya Mall akiwa na begi la nguo. Eti status ameandika “mambo ya shopping upoo!” halafu akaweka na viemoji vya ndege inaruka.
Kwa status ile alizidi kunitia hasira nikaghairi kabisa mpango wa kumnyenyekea na kumpigia magoti. Nikanyanyuka kutoka kitandani na kuvaa nguo zangu  nikabeba na kisu cha jikoni na kunyata ili dada na mama wasisikie kama naondoka, nilipopita karibu na chumbani kwa mama nilisikia akiangusha maombi.

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA

ITAENDELEA JUMATATU

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments