SUMU YA PENZI SEHEMU YA HAMSINI NA SITA (56)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Nilinyanyua simu na kumpigia, akapokea huku nikisikia kabisa sauti yake ikilazimisha furaha baada ya kunisikia.
“mama, kwa nini ulinificha!.. kumbe baba yupo hivyo” niliuliza huku machozi yakinitoka kiasi kwamba hadi Gululi alinishangaa.
Kwa kuwa ilikuwa ni usiku kidogo nilishindwa kurudi nyumbani japo kuwa nilitamani, na isingekuwa vizuri kuondoka bila Bibi. Gululi kuwepo nyumbani pia.
Kwa jinsi nilivyokuwa na huzuni, nilishindwa hata kumjibu Gululi ambaye alikuja karibu yangu na kunibembeleza.
Lakini bado nilikuwa najiuliza inawezekanaje sasa kama mume wangu hahusiki? aliwezaje kufika pale dukani na kumnunulia Fatuma kitenge?
Nikajua siwezi kupata jibu la swali langu kama sitampigia mume wangu, nikamuendea hewani, kama kawaida yake hakuwa akichelewa kupokea hususani kama mimi mkewe ndiye niliyepiga simu, yaani hata kama akiwa anaongea na nani lazima akate tu kwanza na kunisikiliza mimi.
“hallow wife,” alinipokelea kwa bashasha.
“kuna nini kati yako wewe, baba na Fatuma,” niliuliza.
“ooh nadhani nimeshajua sababu ya wewe kuondoka nyumbani. Lakini kwanini uliamua kuondoka wakati ulitakiwa kubaki nyumbani kumbembeleza mama kwa yote yaliyotokea?” alianza kunihubiria sasa; nikatamani kumwambia sikufahamu  hayo kabla lakini nikaamua kuweka swali langu liwe specific zaidi maaana niliona kama hanielewi.

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA

ITAENDELEA JUMATATU

Post a Comment
Powered by Blogger.