SUMU YA PENZI SEHEMU YA HAMSINI NA SABA (57)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Aisee moyo huo mimi sina,  nilikuwa tofauti aisee, kwa muda mchache tu nadhani mmeona nilichoweza kufanya. 
Sasa kwa kuwa mama haongei, mtu mwingine wa kumalizana naye alikuwa ni mume wangu na nilikuwa na maswali mengi mno kwake.
Nilimfuata huko nje nikamuona anacheza na Kendrick, mtoto wangu aliponiona tu akatabasamu na kuongea maneno yake yasiyoeleweka, nikamnyanyua na kumbusu kwa nguvu nikilipiza siku zote ambazo nilikuwa nimemmiss mno.
Nikiwa nimembeba mwanangu, mume wangu naye akawa anakuja eti anikumbatie, nikajitoa kwanza kwa sababu nilitaka anieleze, tena anieleze uzuri, nimuelewe ndipo tuive sahani moja.
“haya kwanza niambie yote uliyosema utanieleza!” nilimwangalia kwa ukali akaanza kunielezea taratibu.
“kiukweli, siku ya pili tu baada ya kufika hapa kwenu, nilianza kuona tabia ya baba yako kuwa siyo nzuri. Kuna kipindi tulipotoka kutembea alikuwa akinitambulisha mademu zake na tena akinitaka niwalipie bili au kuwanunulia vitu mbalimbali. “Nilikuwa sipendi kukwambia lakini I’m so ashamed,” alisema mume wangu kwa uchungu kidogo nikalegeza ukali nikamsogelea na kumshika bega.
“nilikuja kugundua kuwa anatembea na rafiki yako yule mwembamba, na hadi sasa ninavyokwambia, huyo msichana ana mimba changa na baba yako ndiyo anahudumia kila kitu,”

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA


ITAENDELEA JUMANNE

Post a Comment
Powered by Blogger.