SUMU YA PENZI SEHEMU YA HAMSINI (50)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


“Mary una tatizo gani leo?” alisema mume wangu huku akifunga zipu yake na kunitoa pale kwenye lile eneo. Kweli nilithibitisha hana hisia kabisa na mimi na kweli alikuwa ametoka kunisaliti,si kitu kingine.
Hasira zilinipanda nikampiga kofi, nikamuona akishangaa kinafki, nikaingia ndani kwangu kwa hasira nikiwapita mama na baba waliokaa sebuleni wakitazama uchaguzi wa Marekani, nikachukua begi langu na kuondoka bila kujali kama ni usiku au lah.
Mume wangu aliyekuwa nje bado akijiuliza kwa kile kibao, alinishangaa nikimpita nikiwa na  begi langu dogo mkononi.
“Mary! Nini kinaendelea? Unaenda wapi?” alisema Jermaine huku akijitahidi kunizuia lakini hapana sikutaka hata kidogo kuongea naye, lakini alinilazimisha nikaropoka. “Najua kila kitu kinachoendelea y’all jus bunch of hipocrates! Wote wanafki wakubwa!”
Baada ya kutupa dongo hilo nikamuona ameganda pale aliposimama kama amelowa maji ya baridi. Nikamuona mama ametoka nje na baba wakihangaika kuniita lakini sikugeuka wala kutazama nyuma nikaenda moja kwa moja barabarani na kupiga simu kwa Hadija.
Alipokea nikamuelezea kuwa nimegombana na mume wangu na nimeondoka nyumbani, nikamuomba japo nilale kwake kwa siku hiyo tu, akakubali na kunielekeza.
Basi nikapanda pikipiki hadi Mwananyamala nyuma ya Hospitali. Nikampigia akatoka nje na kunipeleka kwenye chumba alichopanga.

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWAITAENDELEA JUMANNE
Post a Comment
Powered by Blogger.