SUMU YA PENZI SEHEMU YA AROBAINI NA SABA(47)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Baada ya kushuka mwenzangu akaanza kuongea na simu kwa ajili ya kuelekezwa kwa kwenda, basi palepale kituoni Chanika Mwisho tukasubiri, akatumwa mtoto mmoja hivi akaja kutuchukua, tukaanza kuingia ndanindani.
Kwa umbali wa dakika chache tukawa tumefika kwenye nyumba moja iliyomaliziwa vyumba viwili tu huku upande mwingine ukiwa na nyumba ya udongo.
Tukamsalimia mwenyeji wetu ambaye ni mdada mmoja hivi saizi yetu mimi na Hadija. Yule mdada akiwa ametuchangamkia akatueleza kuwa Bibi Gululi alikuwa anaoga hivyo tumsubiri hapo sebuleni. Sasa mimi akili yangu ikadhania kuwa huyo Bibi Gululi alikuwa bibi haswaa, lakini nilishangaa alipokuja maana japo alikuwa mtu mzima lakini hakuwa mzee kiasi hicho.
Alipofika alitusalimia lakini kwa Hadija alimchangamkia kweli hadi wakakumbatiana nikathibitisha kuwa kweli walikuwa wakifahamiana kwa muda mrefu, basi akatutaka tusubiri mara moja wakati yeye anaingia ndani na kuvaa. 
Kilichonishangaza mimi ni kwamba yule bibi akiwa hukohuko chumbani, nikasikia akimuita yule mdada na kumtaka ampelekee moto kwenye chetezo, alipopelekewa nikasikia harufu ya udi ukifukizwa.
Hadija aliyejiachia pale ndani kama kwake, akasema kwa sauti; “Mh Bibi Gululi kumbe na wewe haujambo?”


UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA


ITAENDELEA JUMAMOSI
Post a Comment
Powered by Blogger.