SUMU YA PENZI SEHEMU YA AROBAINI NA SITA(46)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Nakumbuka siku hiyo nililala nikiwa nina donge zito moyoni sikuwahi kuwa hivyo tangu nizaliwe. Hata nilipopitiwa na usingizi sikuwa najijua. Hatimaye niliamka asubuhi nikiwa nimechelewa mno tofauti na siku nyingine ambapo huwa naamkaga mapema na kwenda kutayarisha kifungua kinywa na kumuogesha Kendrick.
Siku hiyo nadhani mama na dada ndiyo walikuwa wanachakarika jikoni maana nilisikia kukurukakakara za vyombo. Wakati naenda nikasikia mama anaongea: “ndiyo hivyo nakwambia ole wako umwambie Mary, kama hauna kifua sema kabisa mapema, sitaki familia ivunjike kwa sababu yako! Umesikia!”
“Nimesikia ndiyo, lakini mimi nahisi Mary anajua, wewe unafikiri rafiki zake hawajamwambia hadi leo!” alisema dada nikajiuliza wanachoongelea ni nini?
“Hajui chochote, rafiki zake wote niliwaonya kama ninavyokuonya wewe. Siku ile yeye alikuwa amelewa na mapema kabla ya tukio  alirudishwa kulala, usitafute sababu ya kumwambia!” alisema mama akionekana hana utani hata kidogo kwa aliyokuwa akiyaongea.
Hapo moja kwa moja akili yangu ikanituma kuwa ilikuwa ikizungumziwa siku ambayo nililewa na kurudishwa nyumbani, nikajiuliza huenda tukio la mume wangu kufanya mapenzi na Fatuma kule kwenye migomba lilijulikana na hapo familia nzima ilikuwa inanificha.

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA

ITAENDELEA IJUMAA
Post a Comment
Powered by Blogger.