Ray Kigosi afunguka kuhusu Mimba na mapenzi yake na Chuchu Hans

Zikiwa zimebaki siku kadhaa msanii wa filamu nchini Chuchu Hans kujifungua msanii Ray Kigosi amefunguka na kumuomba Mungu mpenzi wake huyo ajifungue salama.


Ray amesema licha ya kupitia mambo mengi lakini Mungu amewapigania mpka sasa wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza kati ya mwezi huu wa kwanza kama siyo wa pili mwanzoni.

Ray Kigosi anasema ulikuwa ni kama utani vile lakini tayari leo umeshafika mwezi wa tisa toka mchumba wake huyo amepata ujauzito huo. 


"Kwanza kabisa napenda kumrudishia sifa na utukufu Mungu baba Muumba wa mbingu na ardhi tumepitia vingi vikwazo lakini yeye atutiaye nguvu aliendelea kusimama na sisi imara asante sana Mungu kwa kuwa mwema kwetu mengi yalisemwa juu yetu lakini Mungu baba umejibu ulikuwa mwezi mmoja kama utani vile hatimaye imefika miezi tisa na sasa kubaki siku chache. Nakuombea my lovely Mzungu Mungu akufanyie wepesi". Ray Kigosi

A photo posted by vicenti kigosi (@ray_kigosi) on
Post a Comment
Powered by Blogger.