PROF. MBARAWA AITAKA NIT KUENDANA NA MAGEUZI SEKTA YA UCHUKUZI

 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwahutubia Wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam. 
 
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Zacharia Mganilwa akiwahutubia Wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam. 
 
Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Blasius Bavo Nyichomba akiwahutubia Wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam. 

Serikali imekitaka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), kuboresha mitaala yake ili kuendana na mageuzi makubwa yanayofanywa katika sekta ya uchukuzi hapa nchini.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema hayo leo katika mahafali ya 32 ya Chuo hicho na kusisitiza kuwa Serikali itatoa nyenzo zote stahiki kwa chuo hicho ili kukiwezesha kutoa wanafunzi watakaokuwa na soko ndani na nje ya nchi.
“Tumeanza kufanya mageuzi makubwa katika Sekta ya Uchukuzi ambapo tayari tumenunua ndege katika mkakati wa kuboresha usafiri wa anga na hivi karibuni tutaanza ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge), itakayowezesha treni ya kisasa naya mwendo kasi kutoa huduma kwa kuanzia Dar es salaam hadi Morogoro”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Amesema reli ya kisasa itakuwa inatumia umeme ili kuwa na mwendo kasi wa kilomita 160 kwa saa na hivyo kuwezesha usafiri wa Dar es Salaam-Morogoro kuwa wa chini ya muda wa saa mbili.
Amesisitiza awamu ya kwanza ya ujenzi wa reli hiyo utaanza hivi karibuni mara baada ya taratibu za kumpata mzabuni wa ujenzi huo kukamilika.
Amebainisha kuwa katika mwaka wa fedha ujao, Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kukarabati ujenzi wa miundombinu ya chuo hicho ili kukiwezesha kuwa cha kisasa na kitakachotoa elimu bora katika ukanda wa Kusini mwa Afrika na kuhakikisha wahitimu wa fani ya ‘Logistics na Transport Management’ wanapata bodi ya kitaaluma ili kuratibu fani hiyo .
“Hakikisheni mnaimarisha utawala bora, utafiti, ushauri wa kitaalamu, machapisho na huduma yenu iwe ya viwango vya ubora ili kuwezesha wahitimu wenu kupata soko pindi wanapohitimu”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa amewataka wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata kwa juhudi, bidii na maarifa ili kuleta manufaa kwao binafsi na Taifa kwa ujumla.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo hicho Prof. Blasius Nyichomba amewataka wahitimu kuendela kujifunza wawapo sehemu za kazi ili wawe watendaji bora na kujiepusha na  majanga ya utumiaji wa madawa ya kulevya, ulevi na ukimwi ambavyo vina athiri wataalamu wengi hapa nchini.
Ameongeza kuwa Chuo hicho kina mpango wa kuanzisha mfumo wa uatamiaji wanafunzi ili kuwawesha wahitimu kupata ajira mara wamalizapo masomo yao.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Prof. Zacharia Mganilwa amesema idadi ya Wanafunzi katika chuo hicho imeongeza kutoka 3500 mwaka 2014/15 hadi kufikia 5340 mwaka huu na wahadhiri wameongezeka kutoka 63 mwaka 2012 hadi 167 mwaka 2017.
Zaidi ya wanafunzi 1,029 wamehitimu Shahada ya Uzamili, Stashahada ya Uzamili, Shahada na Diploma katika fani mbalimbali za usafirishaji na menejimenti zitolewazo katika Chuo hicho.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Wahitimu pamoja na Viongozi mbaimbali wakiwa katika maandamano kuelekea viwanja vya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa ajili ya kumpokea mgeni rasmi na shughuli ya mahafali kuanza chuoni hapo leo 27/01/2017 jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (katikati) akiwa ameongozana na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Zacharia Mganilwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Blasius Bavomara baada ya kupokelewa na Bendi ya Jeshi la Polisi kuelekea kwenye viwanja vya chuo tayari kwa ajili ya kuanza sherehe ya mahafali ya 32 ya chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) 27/01/2017 jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Zacharia Mganilwa wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya Wahitimu wa kozi mbalimbali toka chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakisikiliza hotuba za Viongozi mbalimbali wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa(aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa kozi mbalimbali toka chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) mara baada ya kuwatunuku Stashahada ya Uzamili, Shahada, Stashahada na Astashahada wahitimu hao leo 27/01/2017 jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa(aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) pamoja na Wafanyakazi wa chuoni hapo mara baada ya mahafali yaliyofanyika leo 27/01/2017 jijini Dar es Salaam. (Picha/Habari na Benedict Liwenga-WHUSM)
Post a Comment
Powered by Blogger.