NGASSA: YANGA INAKOSA WACHEZAJI WAWILI MUHIMU SANA

Kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa amesema kwamba Yanga inahitaji wachezaji wawili wa kuchezesha timu ili kuwa na uwiano mzuri kikosini.
Ngassa ambaye kwa sasa anachezea Mbeya City, alisema leo katika mahojiano kwamba Yanga inahitaji wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kuuchezea mpira na kutoa pasi za mwisho.  

“Ukiangalia Yanga wanavyocheza kwa sasa, unaona kabisa inakoa watu kama wawili wa kuchezea mpira na kutoa pasi za mwisho kama alivyo Niyonzima (Haruna). Ili wawe na uwiano mzuri katika timu, lazima wawapete hao watu,”alisema.

Maoni hayo ya Ngassa yanafuatia Yanga kufanya vibaya katika michuano ya Kombe la Mapinduzi wakitolewa na Simba SC kwa penalti 4-2 Jumanne usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibat baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.

“Mechi ilikuwa nzuri, Simba waliwazidi katikati Yanga, ambao walikuwa wanacheza mipira mirefu kumtumia Msuva (Simon) peke yake, hivyo Simba wakagundua njia hiyo, baada ya kusogea pembeni mipango wakauwa,”alisema.

Pamoja na hayo, Ngassa alisema kwamba wachezaji wengi wa Yanga kwa sasa wamechoka baada kucheza mashindano mengi mfululizo msimu uliopita, hivyo wengi wao miili yao imechoka.
Post a Comment
Powered by Blogger.