MKUU WA WILAYA AMFUKUZA MHANDISI RAYMOND SWAI KWENYE MRADI WA DARAJA LA TAGAMENDA

Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela(kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Dr. William Mafwele, mwenye miwani ni mhandisi wa Manispaa, Eng. Lihamba .

Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela leo alitembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Tagamenda linalofadhiriwa na serikali ya Uingereza kupitia shirika lake la DFID. Wakati wa ziara hiyo aliyoongazana na Mkurugenzi wa manispaa ya Iringa Dr William Mafwele pamoja na mhandisi wa Manispaa, Eng. Lihamba.
 Akipokea taarifa ya kazi, aliambiwa kuwa Mhandisi msimamizi wa Mradi amekuwa kikwazo cha utendaji na utekelezaji wa majikumu ikiwemo hata kunyanyasa wafanyakazi. Ndio maana mradi umekuwa unasua sua.
 Mkuu wa wilaya aliamuru Mhandisi Raymond Swai aondolewe haraka na asikanyage kabisa eneo la mradi akionekana mita 100 achukuliwe hatua. " OCD mtafute haraka Raymond Swai mpe amri amri hii kama anabisha atatakiwa aondoke Iringa" Alisema Mkuu wa wilaya. Muda huo saa 5 asubuhi bado Mhandisi huyo alikuwa hajafika kazini kufanya kazi na kupelekea kazi kutoanza kwa wakati.
Mkurugenzi wa Manispaa Dr Mafwele alionyesha wasiwasi wa mradi kumalizika kwa wakati kwani mkandarsai amekuwa anaishiwa vifaa mara kwa mara . Mkuu wa wilaya alimuagiza Mkandarasi kuleta vifaa haraka wiki ijayo atapita kukagua tena. 
Mradi huo wenye thamani wa 5.3 bilioni unatarajiwa kukamilika mwisho wa mwezi wa 3 kama makandarasi atafuata ratiba.​
Post a Comment
Powered by Blogger.