MKUU WA MKOA AMVUA MADARAKA AFISA ELIMU WILAYANI MBINGA

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge amemvua madaraka Afisa Elimu sekondari wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma mwalimu Oscar Kumburu kwa kosa la uzembe na kushindwa kuwa na takwimu za wanafunzi walioripoti kidato cha kwanza.
Mkuu huyo wa mkoa amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga Bw.Gombo Semandito kumvua madaraka afisa elimu huyo mwalimu Kumburu baada ya kushindwa kumuwasilishia takwimu za wanafunzi walioingia sekondari.

Awali mkuu huyo wa mkoa alikagua maendeleo ya wanafunzi walioripoti sekondari,awali na darasa la kwanza ambapo idadi ya wanafunzi walioripoti  haikumridhisha.

Dkt Mahenge amesema kuwa jukumu la kumnunulia mtoto sare za shule ni jukumu la mzazi na mzazi anaposhindwa kutimiza wajibu huo anapaswa kufunguliwa kesi vinginevyo awe katika kundila maskini waliokidhi vigezo vya umaskini.
Post a Comment
Powered by Blogger.