MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI, IGP ERNEST MANGU ATUMA TIMU YA MAOFISA WA JESHI LA POLISI KWENDA ZANZIBAR KUCHUNGUZA VITENDO VYA UDHALILISHAJI

Msemaji wa Polisi, Advera Bulimba – ACP

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu ametuma timu ya Maofisa  wa Polisi ikiongozwa na Kamishna wa Polisi Jamii Mussa Alli Mussa kwenda Zanzibar kushughulikia kero na malalamiko ya wananchi juu ya vitendo vya udhalilishaji na ukatili kwa watoto/wanawake ambavyo vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara.

Timu hiyo imepewa jukumu la kuchunguza vitendo hivyo vya udhalilishaji na kiini chake na hatimaye kuja na mpango mkakati wa kuzuia vitendo hivyo ikiwemo kuwakamata  wahusika na kuwafikisha mahakamani.

IGP Mangu amewataka wananchi wa Zanzibar, Taasisi za kiserikali na Taasisi za kiraia zilizopo Zanzibar kutoa ushirikiano kwa timu hiyo ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na maadili ya Watanzania.

Imetolewa na:
Advera John Bulimba - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi. 
Post a Comment
Powered by Blogger.