MATANGAZO....
pamoja blogBABA

HABARI

MATUKIO

Michezo imedhaminiwa na

MICHEZO

Simulizi zimedhaminiwa na

SIMULIZI

JAMII

BURUDANI

UCHUMI

MAGAZETI

VIDEO ZETU

» » » MIKE MUSHI AONGEZWA KESI MMILIKI WA JAMII FORUM


Pamoja Blog 1/26/2017 02:29:00 PM 0


Mwanahisa wa Jamii Media Co Ltd, Mickey William ameunganishwa katika kesi mbili zilizokuwa zinamkabili mkurugenzi mtendaji wa mtandao huo, Maxence Mubyazi za kuzuia uchunguzi wa jeshi la polisi.
Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka hayo leo mbele ya hakimu mkazi mkuu, Thomas Simba na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa.
Wakili wa Serikali, Mohammed Salum alidai kuwa washtakiwa hao wakiwa katika eneo la Mikocheni kwa nafasi zao na wakijua jeshi la polisi linafanya uchunguzi kuhusiana na mawasiliano ya kimtandao ambayo yalichapishwa katika tovuti yao kwa njia ya kuzuia uchunguzi huo walishindwa kutekeleza amri ya kutoa data walizonazo.
Upelelezi wa kesi hizo umekamilika washtakiwa watasomewa maelezo ya awali Februari 9 na 20, 2017. Washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments