MAMA WA MTOTO ZAHARA ALIYEASILIWA NA ANGELINA JOLIE AOMBA KUKUTANA NA MWANAE

Angelina Jolie alimchukua Zahara akiwa na miezi sita tu

Zahara alikuwa dhaifu, mwenye utapiamlo na aliyezungukwa na umaskini wa hali ya juu katika familia yake.
Akiwa na miezi 6 tu, Angelina Jolie aliingiwa imani na kuamua kumchukua na kumuasili, kumfanya kama mwanae wa kumzaa.
Angelina Jolie aliwahi kudai kuwa aliambiwa mama yake Zahara alifariki kwa ugonjwa wa Ukimwi 2005 alipomchukua. Ukweli ni kuwa mama yake alikuwa hai

Sasa Zahara amekua na ana miaka 12 huku akiishi maisha ambayo kila mtu anayaota akiwa na mzazi wa kumlea tajiri.
Zahari ana umri wa miaka 12 sasa

Na sasa mama yake mzazi na Zahara, – Mentewab Dawit Lebiso wa Ethiopia ana hamu kubwa ya kumuona mwanae.
Mentewab Dawit Lebiso, mama mzazi wa Zahara

Licha ya kuwa Mentewab anakiri kwamba Angelina amefanya kazi kubwa kumlea mwanae, anaomba tu japo nafasi ya kumuona kidogo. “Nataka tu ajue kuwa mimi ni mzima na nina hamu kubwa ya kuongea naye. Sihitaji kumchukua mwanangu, lakini ni walau tu kuwa naye karibu, kumuita na kuongea naye,” aliiambia Mail Online.
“Angelina amekuwa zaidi ya mama kwake kuliko mimi ambavyo ningekuwa. Amekuwa naye tangu akiwa mtoto, lakini hiyo haimaanishi kuwa simmiss. Nammiss muda wote. Namfikiria kila siku na nina hamu ya kusikia sauti yake na kuona sura yake.”
Mentewab bado anaishi maisha duni sana

“Najua siku anapokuwa na birthday lakini nina huzuni sababu siwezi kusherehekea naye. Ningependa sana kusherehea naye kwenye siku yake ya kuzaliwa na siku zake muhimu zingine. Ninatamani ya kuwa na uwezo wa kuwasiliana naye mara kwa mara.”
Aliendelea, “Ningependa Zahara ajue kuwa ana mama ambaye anampenda kama Angelina. Najua maisha yake na Angelina yapo kwenye nchi nyingine na anazungumza lugha nyingine kuliko mimi. Ana maisha ambayo nisingweza kumpa, lakini bado ningependa kuwasiliana naye.”

“Ningependa kuona sura yake. Amekuwa msichana mrembo na ninajivunia. Moyo wangu unapasuka sababu ninajivunia. Wote tutakufa siku moja, na kabla sijafa, ningependa ajue kuhusu mimi na kwamba ana familia huku Ethiopia. Ningemuomba Angelina aniruhusu niongee naye. Nadhani si kitu kikubwa sana kuomba.
Post a Comment
Powered by Blogger.