MAJESHI YA SENEGAL YAINGIA GAMBIA KUMNG’OA RAIS KING’ANG’ANIZI YAHYA JAMMEH

Viongozi wa Afrika Magharibi wamempa Yahya Jammeh nafasi ya mwisho kuachia madaraka wakati majeshi ya Senegal yakiingia nchini Gambia tayari kwa kumng’oa.

Jammeh amepewa hadi Ijumaa hii  mchana awe ameshachukua virago vyake ama kuondolewa kwa nguvu na majeshi ya Afrika Magharibi yanayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, Ecowas inamuunga mkono Adama Barrow, aliyeapishwa kama rais mpya wa Gambia, Alhamis hii katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal.

Ni rais halali sababu ndiye alishinda uchaguzi wa mwezi uliopita na amekuwa akitambulika kimataifa. Barrow, ambaye bado yupo nchini Senegal, amedai kuwa hatarejea kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Banjul, hadi pale operesheni ya kijeshi itakapokamilika.
Post a Comment
Powered by Blogger.