MAGUFULI:WATU WALIOBOMOA NYUMBA ZAO KUFUATIA TETEMEKO MKOANI KAGERA HAWATOLIPWA FIDIA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amesema watu waliobomoa nyumba zao mara baada ya tetemeko la ardhi lililotokea septemba 10 mwaka jana mkoani Kagera hawatalipwa fidia yoyote na kwa kuwa walifanya hivyo kwa nia mbaya.

Rais Dokta Magufuli ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Misenyi muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha afya cha Kabyaile wilayani misenyi mkoani Kagera.
Post a Comment
Powered by Blogger.