MADONNA KUCHUNGUZWA KWA KUTOA MATAMSHI MAKALI DHIDI YA TRUMP

Idara ya Upelelezi nchini Marekani imesema itafungua uchunguzi dhidi ya Madonna, baada ya mwanamuziki huyo kusikika akiwaambia Wanawake walioandamana Jijini Washington kwamba alifikiria kuilipua Ikulu kufuatia ushindi wa Donald Trump.

Katika maandamano hayo ya wanawake kupinga sera za Trump, Madonna alitumia matamshi makali yaliyolazimisha vyombo vilivyokuwa vikirusha mubashara tukio hilo kuomba radhi mara kwa mara.

Akiongelea hasira alizokuwanazo baada ya matokeo ya urais, Madonna aliwaambia waandamanaji alifikiria mno kuilipua Ikulu, lakini alijua kuwa kufanya hivyo kusingebadilisha chochote.
            Waandamanaji wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali Jijini Washington DC
              Theron mwenye hisia kali akitokwa na machozi wakati wa maandamano hayo
             Mwanamuziki Alicia Keys naye alishiriki maandamano hayo ya Jijini Washington DC
Mwanamuziki John Legend naye alikuwa miongoni mwa waandamanaji waliounga mkono maandamano hayo ya wanawake 
Muigizaji filamu mkongwe Whoopi Goldberg naye alikuwa ni miongoni mwa walioandamana Jijini Washington DC


Post a Comment
Powered by Blogger.