Lowassa: Mshikamano Ukawa utaing’oa CCM

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa mshikamano wa mwavuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ni hatua kubwa katika kuelekea kuing’oa CCM madarakani.
“Wameanza mbinu zao za kutaka kutuondoa katika umoja wetu, wameanza kuwalisha viongozi wetu maneno,” amesema Lowassa mjini Biharamulo ambaye ameongozana na Naibu Katibu Mkuu Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu.
“Wanaandika uongo mchana kweupe kuwa nilikuwa katika kampeni kwenye kitongoji Ematasia... mimi sikwenda huko, lakini mbinu zao hizi wananchi wameshazijua na hawako tayari kuona hamu yao ya kupata mabadiliko inapotea,” amesema.
Lowassa ambaye ametokea Zanzibar alikoshiriki uzinduzi wa kampeni za ubunge wa Jimbo la Dimani kwa upande wa CUF amesema viongozi wa vyama vya upinzani wana mshikamano mkubwa na kuwataka wanachama wao kuiga mfano huo.
“Katika ziara zetu hizi za kuimarisha chama chetu pia tunaimarisha mshikamano miongoni mwetu sisi wapinzani... CCM wanapata kiwewe na tunawaambia hata wafanyeje mabadiliko hayaepukiki, watawatia ndani viongozi wetu kwa hila lakini wajue hiyo ndiyo inazidisha vuguvugu. Huu ni upepo unaovuma kote duniani hivi sasa wajifunze yaliyotokea Gambia, Ghana na kwengineko,” amesema Lowassa ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, aligombea urais na kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais John Magufuli.
Post a Comment
Powered by Blogger.