KUCHANGANYA POMBE NA VINYWAJI VYA KUONGEZA NGUVU (ENERGY DRINKS) NI HATARI KWA AFYA YAKO

Mchanganyiko wa pombe na vinywaji vya kuongeza nguvu vijulikanavyo kama Energy drinks vilitosha kumfanya akose usingizi na kuwa mwenye nguvu kwa muda wote kipindi alipokuwa akikesha katika kumbi tofauti tofauti za starehe katika katika jiji la Dar es Salaam wakati akisoma katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Lakini leo hii akizungumzia mambo yanayohusu afya yake na yako, kuchanganya pombe na Energy drinks ni jambo ambalo asingekushauri kabisa ulifanye. Kwani hali ya afya yake ipo ukingoni na asingependa kabisa kuona mtu mwingine akiingia katika majanga aliyoyapata yeye.

Je ni kweli vinywaji hivi vijulikanavyo kwa jina la energy drinks huongeza nguvu kama inavyosemekana? Wataalam wa afya wanatoa tahadhari kuhusiana na madhara yatokanayo na hivi vinywaji maarufu. Utumiaji wa vinywaji hivi kwa muda mrefu husababisha matatizo ya moyo ambayo ni hatari sana kwa afya yako.
Utafiti uliofanyika katika nchi nyingi duniani unaonyesha vinywaji hivi vikitumiwa kwa muda mrefu huleta madhara makubwa kwa watumiaji kama vile kuongezeka kwa mapigo ya moyo (Increased heart rate) ambayo hupelekea kuongezeka kwa msukumo wa damu (blood pressure) ambapo mwisho wa siku hupelekea watumiaji kupata shinikizo la moyo (Hypertension) na shambulio la moyo(heart attack).
Kitaalam vinywaji hivi vijulikanavyo kama energy drinks vimechanganywa na caffeine ambayo husababisha mnywaji wa vinywaji hivi kukosa usingizi huongeza uelewa na hupunguza uzito.
Lakini ikitumiwa kwa wingi na kwa muda mrefu,caffeine husababisha addictions na matatizo ya moyo. Kwahiyo ni vema tukaepuka kuchanganya pombe na vinywaji vya aina hii ili kuepukana na madhara yatokanayo na utumiaji wa mchanganyiko huu.

IMEANDIKWA NA:
FORD A. CHISANZA
Intern pharmacist
Tanzania Food And Drug Authority (TFDA)
Mobile:+255 652466430/+255 684363584
Post a Comment
Powered by Blogger.