JE WATAKA KUJUA: MFAHAMU MAKAMU WA RAIS WA ARGENTINA BI GABRIELA MICHETTI.

 Ni mwanamama aliyepata ajali ya gari mwaka 1994, ajali iliyomfanya apate ulemavu wa miguu na kupelekea kutumia kiti cha magurudumu. Mwaka 2007 Bi Gabriela aliteuliwa kuwa mgombea mweza wa Meya Mauricio Macri katika kinyang'anyiro cha umeya na akafanikiwa kuwa Naibu Meya wa kwanza mwanamke wa Jiji la Buenos Aires. 
Mwaka 2015 akateuliwa kuwa mgombea mweza katika uchaguzi mkuu uliomwezesha kuwa Makamo wa Rais wa Argentina, chini ya serikali inayoongozwa na Rais Mauricio Macri (walifanya kazi pamoja kama Meya na Naibu Meya wa Jiji la Buenos Aires). Serikali inayoongozwa na kaulimbiu ya "pobreza cero" yaani "zero poverty", kauli mbiuyenye lengo la kumaliza umaskini mkubwa ulioachwa na serikali ya Rais Cristina Fernández de Kirchner aliyeacha deni kubwa la Dola za Kimarekani Billion 188.7 
Bi Michetti amebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume na mpenzi wake wa siku nyingi mwanahabari Eduardo Cura.

IMEANDALIWA NA MOSES MUTENTE
Post a Comment
Powered by Blogger.