JE WATAKA KUJUA: KUNA NCHI MFUNGWA AKITOROKA GEREZANI SIO KOSA

Nchini Mexico, Ujerumani na Austria sheria inatambua kwamba kila binadamu anatamani kuwa huru hivyo kwa mujibu wa sheria za nchi hizo si kosa la jinai kwa mtu kutoroka gerezani, ingawa sheria zitachukuliwa endapo utasababisha hasara yoyote au madhara wakati wa jaribio lako la kotoroka. 
Mfano endapo utatoroka na kuvunja dirisha na kukimbia ukikamatwa utaongezewa adhabu kwa kosa la kuharibu mali na kuiba sare za gereza (ulizovaa) lakini hautashtakiwa kwa kutoroka. Kosa la kujaribu kutoroka litakuwa na adabu endapo mtu aliyejaribu kutoroka alifanya hivyo kwa msaada wa watu waliopo ndani au nje ya gereza hilo. 
Kifungu cha 154 cha sheria ya Mexico kinasema “mfungwa atayejaribu kutoroka hatakabiliwa na adhabu yoyote isipokuwa pale itakapothibitika kwamba alifanya hivyo kwa msaada wa watu wengine ama alifanya uharibifu wakati wa jaribio hilo na atakabiliwa na kifungo cha miezi 6 hadi miaka mitatu gerezani”

Imeandaliwa na Moses Mutente
Post a Comment
Powered by Blogger.