JE WATAKA KUJUA: "INEMURI" utamaduni unaoruhusu wafanyakazi kulala ofisini nchini Japan.

"Inemuri" utamaduni unaoruhusu wafanyakazi kulala ofisini nchini Japan. Nchi nyingi duniani hata hapa kwetu Tanzania mtu anayekutwa amelala ofisini hutafsiriwa kama mvivu, mzembe, wa hovyo na asiyewajibika. Hata boss wako akikukuta umelala ofisini bila shaka atasikitika sana,

Lakini kwa tamaduni za Kijapani ni jambo la heshima mtu kuonekana amechoka. Mara nyingi mtu aliyechoka hutafsiriwa kama mchapakazi hodari.Huyu mtu amechoka kwasababu amefanya kazi sana. Hivyo kuonekana kwamba umechoka ni jambo la kifahari na ni njia mojawapo ya kutuma ujumbe kwamba wewe ni jembe na ni mchapakazi.

Hivyo ni ruksa kwa mfanyakazi kulala ofisini wakati wa kazi, hata kama kuna kazi zinaendelea, mfano hata kama kuna mtu anafanya presentation (uwasilishaji wa maelezo fulani) wewe unaruhusiwa kudozi. Lakini sharti ni kwamba ukilala unapaswa kulala kwenye kiti ukiwa umenyooka (upright), usijimwage kama vile upo kitandani. Utamaduni huo unatambulika kama Inemuri.

Wafanyakazi wengi wa Japani wanapoagana wakati wa kutoka kazini hawaambiani "uwe na jioni njema" badala yake wao huambiana "otsukaresama deshita" wakimaanisha "Unaonekana umechoka sana". Ni jambo la fahari kuonekana umechoka. Pichani ni Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe na waziri wa fedha wakiwa wamelala katikati ya kikao.

IMEANDALIWA NA MOSES MUTENTE
Post a Comment
Powered by Blogger.