HATIMAYE RAIS YAHYA JAMMEH AKUBALI KUACHIA MADARAKA GAMBIA

Kiongozi wa muda mrefu wa Gambia, Yahya Jammeh, amesema ataachia madaraka, hii ikiwa ni baada ya kukataa kushindwa katika uchaguzi mkuu.

Akiongelea uamuzi wake huo kwenye TV Jammeh, amesema kuwa hakuna umuhimu wa kumwagika hata tone la damu katika nchi ya Gambia.

Kauli yake hiyo inafuatia mazungumzo yaliyodumu kwa saa kadhaa baina ya Jammeh na wasuluhishi wa mataifa ya Afrika ya Magharibi.

Jammeh ameiongoza nchi hiyo kwa miaka 22 lakini alishindwa katika uchaguzi wa mwezi Desemba mwaka jana na mpinzani wake Adama Barrow.

Barrow amekuwa katika taifa la jirani la Senegal kwa siku kadhaa na aliapishwa kuwa rais wa Gambia kwenye ubalozi wa Gambia nchini Senegal siku ya Alhamisi.

Rais mpya wa Gambia Adama Barrow 
Post a Comment
Powered by Blogger.