DR CONGO YAIFUNGASHA VIRAGO NCHI YA TOGO AFCON

Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imetinga katika hatua robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika baada ya kupata ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Togo katika kundi C.

Mfungaji anayeoongoza kufamania nyavu katika michuano hiyo Junior Kabananga aliunganisha pasi ya Chancel Mbemba na kufunga goli lake la tatu katika michezo mitatu.
Mpira wa adhabu uliopigwa na Paul-Jose M'Poku ukijaa wavuni na kuandika goli la tatu la DR Congo

Kabananga tena aligonga mwamba kwa mpira wa kichwa kabla ya Ndombe Mubele kuongeza goli la pili kwa DR Congo baada ya mapumziko.

Kodjo Fo-Doh Laba aliipatia matumaini Togo baada ya kufunga goli, lakini mpira wa adhabu uliopigwa na Paul-Jose M'Poku ulijaa wavuni na kuihakikishia ushindi DR Congo.

Post a Comment
Powered by Blogger.