BENKI YA DUNIA KUIKOPESHA TANZANIA $350M KUPANUA BANDARI YA DAR

Benki ya Dunia imekubali kuikopesha Tanzania fedha kwaajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mkopo wa dola milioni 350 kwa ajili ya mradi wa upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dokta Philip Mpango, amewaambia waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati yake na Makamu wa Rais wa Benki ya dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Makhtar Diop, makao makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
Alisema, “Makamu wa rais wa benki ya dunia wamekubaliana na mheshimiwa rais kwamba benki ya dunia kwaajili ya mradi wa kupanua bandari yetu ya Dar es Salaam, ambao ni mradi utakaogharimu takriban dola milioni 350. Kwahiyo ni mambo makubwa haya ambayo yatatuwezesha sasa kuzifanya biashara kwenda nchi jirani lakini biashara zetu humu ndani ziweze kwenda kwa haraka zaidi na kwa ufanisi zaidi.”
“Kwahiyo ni miradi muhimu sana ambayo benki ya dunia imeonesha utayari kabisa wa kutusaidia na wameahidi sasa wataharakisha michakato ili kazi ianze haraka iwezekanavyo.”
Post a Comment
Powered by Blogger.